MoCU Repository

Neno la Shukrani Kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Mheshimiwa Balozi Nicholaus Kuhanga Kwenye Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara, Moshi Tarehe 18 Machi 2006

Show simple item record

dc.contributor.author Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara, Moshi
dc.date.accessioned 2024-11-19T17:22:18Z
dc.date.available 2024-11-19T17:22:18Z
dc.date.issued 2006
dc.identifier.uri http://repository.mocu.ac.tz/xmlui/handle/123456789/1791
dc.description.abstract Mhcshimixsa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Waheshimiwa Mawaziri, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi Wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi, Viongozi mbalimbali wa Chuo, Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wadau wa Elimu ya Juu, Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wadau wa Ushirika, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana. Mheshimiwa Rais, Kazi yangu kuu leo ni kutoa shukrani kwa kazi uliyomaliza kuifanya sasa hivi, kwani wenzangu wengine wameishazungumza mengi kuhusu tukio hili la leo. Lakini kabla ya kutoa neno la shukrani, ninaomba kuungana na Watanzania wenzangu kukupongeza wewe binafsi na chama cha CCM kwa kupala ushindi mkubwa katika uchaguzi Mkuu uliopita. Ushindi huu umeidhihirishia dunia nzima kwamba wewe, kwa hakika, ni Iulu iliyokuwa ikisakwa na Watanzania. Baada ya pongezi hizi, Mheshimiwa Rais, ninaomba sasa nichukue fursa hii kwa niaba ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara- Moshi kutoa shukurani nyingi kwako, kwanza kwa kukubali kuja kutuzindulia Chuo hiki kipya. Mheshimiwa Rais, tulipokuwa tunafanya mipango ya kukualika hapa, tulisita kidogo na kuwa na wasiwasi. Tulisita kwa sababu tulijiuliza mara nyingi kama kweli itawezekana wewe kuja hapa binafsi katika kipindi ambacho ndio kwamba unaanza kazi yako mpya na ngumu ya kulihudutnia hili. Lakini 2 tulijipa moyo kwa kusukumwa no imani yetu kwako kwa kuwa Rais anayejali ntatukio yoyote ya kimaendeleo, kama hili tunaloshuhudia leo. Kwa mtu mwenye kazi nyingi kama wewe, yumkini ulikuwa umeshaandaa ratiba yako ya kazi na mambo muhimu ya kufanya. Tunajua, kwa uhakika, kwamba mwaliko wetu haukuwepo Kwenye rativba ya kazi zako. Kwa hiyo, inaleta faraja kuona kuwa mara mwaliko ulipkufikia uliufikiria na kwa upendo wako mkubwa ukauweka Kwenye ratiba ya kazi zako. Mheshimiwa Rais, hii peke yake ni ushahidi wa kutosha wa jinsi unavyothamini jitihada mbalimbali za wananchi na taasisi zao za kutaka kuimarisha huduma kwa Watanzania. Kukubali kwako kuja kuzindua Chuo hiki ni uthibitisho kuwa unaafiki juhudi na michango ya watu na taasisi mbalimbali katika mchakato wa kukifikisha Chuo hiki katika hadhi yake ya sasa. Kwa niaba ya wadau na wote wanaokitakia mema Chuo hiki, ninasema "ahsante sana kwa kukubali mwaliko wetu". Aidha, Mheshimiwa Rais, Sisi tuliobahatika kualikwa kushuhudia tukio hili kubwa, tumefarijika kupata nafasi ya kukuona na kukusikia ukiongea kwa karibu, na hasa ukiwa ni kiongozi wa Ngazi ya Juu kabisa hapa nchini. Ukubwa wa umati uliohudhuria hapa unadhihirisha kuwa Watanzania wengi bado wana shauku kubwa ya kukusikiliza na kukuona kwa karibu. Ujii wako hapa ni furaha kwa watu wengi wa Mkoa wa Kilimanjaro na majirani zao. Kwa hiyo, ungekataa mwaliko wetu, umati wote huu hapa ungebaki umefadhaika. Pili, Mheshimiwa Rais, uzinduzi wa leo ni kumbukumbu muhimu uliyoiweka katika historia ya Elimu ya Juu hapa nchini. Tumepata fursa ya kusikia nasaha zako, maagizo yako, matarajio yako na changamoto mbalimbali zinazoihusu sekta ya Elimu ya Juu kwa ujumla na Sekta ya Ushirika. Kwa jinsi baadhi ya changamoto hizo zilivyonigusa binafsi, ninaomba nirejee baadhi yake hapa. Changamoto mojawapo ilihusu vigezo vya kuzingatia wakati taasisi mbalimbali zinapoamua kuanzisha Vyuo vya Elimu ya Juu. Ni kweli, Mheshimiwa Rais kama ulivyosema, kuna hatari ya kuanzisha vyuo vikuu kama fasheni. Ukisikia, mathalan, nchi fulani wameanzisha Chuo Kikuu cha Unajimu na Sayansi za Nyota, haraka haraka na wewe unaanzisha Chuo Kikuu cha Sayansi ya Mwezi na Jua! Wahitimu wakimaliza programu hizo za Nyota na Jua wanakuwa kama samaki aliyetolewa baharini na kuwekwa ardhini nchi kavu! Hawawezi kusaidia watu wao katika maendcleo. Huu utakuwa ni upungufu mkubwa kwa wadau na wahusika wengine katika kubuni mikakati ya maendeleo halisi ya Watanzania. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Moshi University College of Co-operative and Business Studies en_US
dc.subject Shukrani en_US
dc.subject Mwenyekiti en_US
dc.subject Baraza en_US
dc.subject Uzinduzi en_US
dc.subject Ushirika en_US
dc.subject Biashara en_US
dc.title Neno la Shukrani Kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Mheshimiwa Balozi Nicholaus Kuhanga Kwenye Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara, Moshi Tarehe 18 Machi 2006 en_US
dc.type Other en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search MoCU IR


Advanced Search

Browse

My Account