Abstract:
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,
Waheshimiwa Mawaziri,
Mheshimiwa Gaudentia Kabaka, Naibu Waziri wa
Elimu va Juu, Sayansi na Teknolojia
Dkt. Naomi Katunzi, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia,
Mheshimiwa Mohamed Babu, Mkuu wa Mkoa,
Ndugu Al Noor Kassim, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo,
Balozi Nicholaus Kuhanga, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoinecha Kilimo,
Prof. Anselm Lwoga, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,
Prof. Chambo, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara,
Ndugu Waalikwa,
Wanajumuiya ya Chuo,
Mabibi na Mabwana.
1. Awali ya yote, napenda kuchukua nafasi hii kwa kuungana na Uongozi wa Chuo kwa kutoa
pongeza za dhati kwako Mheshimiwa Rais kwa ushindi mkubwa ulioupata kaıika uchaguzi
uliofanyika tarehe 14 Desemba, 2005 na hatimaye kuteuliwa kuwa Rais wa Jumhuri ya
Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Nne. TUNASEMA HONGERA.
Mheshimiwa Rais, uongozi wako wa takriban miezi mtatu, tayari umekwisha, kuna na kuwagusa
wananchi walio wengi hasa pale ambapo umeamua kutembelea binafsi kila Wizara kuona shughuli zao na haıimaye kutoa maagizo rami badala ya kukaa Ikulu na kusubiri laarifa kuloka kwa
Watendaji. Huu ni uongozi wa kulembelea maeneo husika (Management by Walking, MBWA) ni
wa kipekcc. TUNAKUPONGEZA SANA.
2. Pili , niruhus nichukue nafasi hii ya pekee kwa niaba yangu mimi mwenyewe na kwa niaba ya
Jumuiya ya Chuo hiki kutoa shukrani za dhati kwak kwa kukubali licha ya shighuli nyingi ulizo
nazo za taifa na kimatifa kuja kuzindua rasmi Chuo hii. TUNASEMA AHSANTE SANA!
3. Mheshimiwa Rais, Uzinduzi wa Chuo hiki Kikkuu cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS)
unafanya jumla ya Vyuo Vikuu vya Umma kuwa VITANO na Vyuo Vikuu vya Vishiriki vya Umma
kuwa VITANO. Aidha, napenda kukufahamisha ya kwamba kuna Vyuo Vikuu binafsi KUMI na
Vyuo Vikuu Vishiriki binafsi TISA, hivyo kufanya Vyuo Vikuu nchini kufika 29. Kutokana na
ongezeko Ia idadi ya vyuo vikuu, kumekuwepo na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojiunga
na vyuo vikuu Kutoka 17,323 mwaka 2000/01 hadi kufikia 36,870 mwaka 2004/05, ikiwa ni
ongezeko Ia wanafunzi 19,547 (53%). Hivyo uzinduzi wa Chuo hiki leo unadhihirisha azma va
serikali ya kupanua Elimu ya Juu kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi Chama cha
Mapinduzi ya mwaka 2005 yenye lengo Ia kuwawezesha asilimia 12.5% ya wanaomaliza Kidato
cha Sita kupata nafasi ya kuendela na masomo katika Vyuo Vikuu, taasisi za Teknolojia na Taasisi
nyingine za Elimu va Juu.
4. Mheshimiwa Rais, Wizara imezingatia maagizo yako uliyoyatoa ulipotembelea Wizara ya Elimu
va Juu, Sayansi na Teknolojia tarehe 01 Februari, 2006 kwamba katika kupanua elimu ya juu,
tuhakikishe kuwa vyuo vilivyokuwa vikitoa mafunzo YA kati vinaendelea kuFanya hivyo badala ya
kuvigeuza vyote kuwa Vyuo Vikuu kwani wahitimu wa mafunzo ya kati bado wanahitajika kwa
maendeleo ya nchi vetu.
5. Mheshimiwa rais, kutokana na maelezo hayo hapo juu, nafurahi kukufahamisha ya kwamba Chuo
hiki kitaendelea na mafunzo yaliyokuwa yakitolewa awali kabla va kupanda hadhi ya kuwa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.
Aidha, upandaji huu wa hadhi ya Chuo hiki umekiongezea uwezo wa kutoa mafunzo hayo katika
ngazi za Cheti, Stashahada ya Kawaida, Stashahada ya Uzamili, Shahada, Shahada ya Uzamili na
Shahada ya Udaktari wa Falsafa. Napenda kukuhakikishia ya kwamba mafunzo yote yanayotolewa
kakika Chuo hiki yanalenga kuondoa umaskini miongoni mwa Watanzania kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005.
6. Mheshimiwa Rais, baada ya kusema hayo machache, kwa heshima na taadhima, sasa nakuomba
nikukaribishe uweze kuzungumza na umma huu na hatimaye kutoa tamko Ia kukizindua rasmi
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA USHIRIKA NA BIASHARA.